Skip to main content

Posts

PANDASHUKA KATIKA SAFARI YA UANDISHI WA HABARI KATIKA CHUO KIKUU

 Bilashaka wanasema kila safari huanza na hatua moja na vilevile katika kila hatua hakukosi changamotowe. Chuo kikuu ni mojawapo ya matamanio ya kila mwenye ari ya masomo kufikia ila kupitia vikwazo mbalimbali sio wote hufaulu katika safari hii kwani wengi hulazimika kuachisha safari hii katikati au pia kukosa nafasi kabisa ya kuianza. Fauka ya hayo, binafsi nimefaulu kuanza masomo kwenye ngazi ya stashahada ya uanahabari katika chuo kikuu cha kiufundi cha Mombasa na kufikia sasa nimekamilisha safari hii kwa asilimia 99. Sio kumaanisha kwamba maisha yamekuwa mtelezo ila changamoto zimekuwepo kiasi cha kukatishwa tamaa na maneno ya wanafunzi wenzangu. Picha kwa hisani ya Okwonko Dhana iliyopo kwa wengi walio nje ya masomo ya vyuo vikuu ni kwamba kila mwenye kufika katika chuo kikuu kwa ngazi yoyote, ni mtu mzima na kwa njia moja au nyingine ana uwezo wa kjisimamia kwenye matumizi yake ya kifedha bila ya kumtegemea mtu yeyote wakiwemo wazazi. Ni vigumu kuamini ila katika ...
Recent posts

DHIMA YA VIJANA KATIKA KUIMARISHA UCHUMI WA KENYA

  Hivi karibuni Taifa la Kenya limeingia katika uchumi wa kati ambalo ni jambo muhimu sana katika mtazamo wa kusonga mbele na kuimarisha tena Uchumi wa Taifa hili ambao umelemazwa tangu kuzuka Kwa janga la Covid 19. Photo cortesy of opera Kijana ni mwanajeshi wa mstari wa mbele katika vita ya kiuchumi na hivyo ikiwa kijana hata shiriki katika shughuli za kiuchumi ambazo zina wezesha serikali kuu kukusanya mapato,kijana huyo anakuwa ni mwanajeshi atumikaye kulidondosha Taifa lake kiuchumi hasa ikizingatiwa kuwa anazo nguvu za kutumika katika nafasi ya kulisaidia Taifa lake Kenya kukua kiuchumi ivyo akiwa hatumiki ndani ya Taifa kwa shughuli za kiuchumi atakuwa  analemaza uchumi kwa Taifa. Kijana anapaswa kuzingatia  kuwa kuwa ikiwa kuna kupanda kwa uchumi wa Nchi  pia kuna kushuka kwa uchumi wa Nchi. Hivyo basi tunapokuwa tungali bado vijana na tuna nguvu ni muhimu kujua kuwa uchumi wa Taifa letu lipo mabegani Mwetu . Photo cortesy of nation media Hivyobasi uchumi wa ...

Mabadiliko ya tabia nchi na athari zake

  Tabia ya nchi ni mwenendo wa hali ya hewa yakiwemo majira, wastani na vizio vya juu na chini kabisa vya joto, utokeaji na mtawanyiko wa mawingu, mvua na theluji, majanga yanayosababishwa na hali ya hewa kama vile upepo mkali na kuanguka kwa theluji, na vimbunga vikali vya nchi kavu na baharini. Tabia ya nchi duniani inabadilika kwa sababu ya kile kinachojulikana kama ‘athari zilizoongezwa nguvu za miali ya jua’. Image Courtesy of google Uhai unawezekana Duniani kwa sababu ya nishati ya jua ambayo hufika katika umbo la mwanga. Dunia huakisi sehemu ya mwanga huu ambao hatimaye hupotelea angani. Hata hivyo, gesi zilizoko kwenye anga hupunguza kasi ya kupotea huku kwa mwanga. Kwa pamoja, gesi hizi hujulikana kama ‘gesi za kuzuia miali ya jua’, kwa Kiingereza, ‘greenhouse gases’, kwani kazi yake ni kuzuia joto lisipotee Duniani. Hii ni kama inavyoonekana katika nyumba maalumu zilizofunikwa kwa nailoni wanazotumia wakulima ili kuotesha mbogamboga. Kiasi fulani cha gesi hizi ni muhimu i...

UCHUMI WA WANAMOMBASA BANDARINI

 Halmashauri ya bandari nchini KPA ni moja wapo ya Mashirika ya serikali yanayotoa fursa nyingi za ajira Kwa wafanyikazi wa umma na wa sekta binafsi kushamiri katika taaluma na idara mbalimbali kujipatia riziki. Wanaonufaika pakubwa wakiwa wakaazi wa Kaunti ya Mombasa ambao rasilimali hii iko katika gatuzi Lao.Miongoni mwa biashara zinazodhamiri katika Kaunti ya Mombasa kutokana na uwepo wa banadari ni pamoja na biashara za kupokea mizigo bandarini na kuisafirisha, ile ya magari za kusafirisha mizigo, biashara za hoteli na zingine ndogo ndogo. (Photo courtesy of KPA website) Lakini awali agizo la kuhamishwa Kwa baadhi ya Huduma muhimu za halmashauri hiyo Hadi katika bandari ya nchi Kavu eneo la Naivasha Kaunti ya Nakuru liliwatatiza maelfu ya wafanyikazi kazi wa sekta binafsi hususan madereva wa malori wa kampuni binafsi ambao hutegemea pakubwa kujipatia mapato kupitia kipato kutokana na shughuli ya usafirishaji wa makasha ya mizigo kutoka bandari hiyo Hadi Mataifa mengine...

How to deal with baneful relationships

Relationships are always interesting and fun when they are smooth and it feels very interested when your partner is also your friend. However, if relationship starts becoming toxic between partners and still percevere, it brings an image of slavery and many find it difficult to cope and end in engaiging in acticities that put them into regrets afterwards. No one wants to find themselves in relationships that are full of quarrels, misunderstandings and traumatizing. However, they rather get out of such relationships when it is too late. When someone finds it difficult in relationship especially for the campus students, their natural reaction in such is to avoid dealing with situation. However its good to know how to deal with such toxic relationships  Bellow are some of the reasons why campus students find rough times in their toxic relationships and still tolerate : 1.Viewing toxity as normal Most people get themselves in abusive relationships and not able to know how to cope with ...

HOFU YA EBOLA NCHINI KENYA

 Kufuatia kudhibitishwa kuwepo kwa virusi vya Ebola nchini Uganda mnamo tarehe 19 mwezi wa tisa 2022 , wizara ya afya nchini humo sasa yawataka waadhiriwa licha ya kupokea matibabu, kuepuka tendo la ndoa angalau kwa siku tisini. Haya yanajiri baada ya kubainika kwamba virusi hivi bado vinaenea hata baada ya muadhiriwa kupokea matibabu hivyo basi kusambazwa sio kwa njia ya mate na damu pekee ila wanasayansi sasa wanabaini kuna uwezekano wa virusi hivyo kupatikana kwenye manii (semen) ya mwanaume hata baada ya kupata matibabu dhabiti. Haya yaanjiri baada ya watu 36 kudaiwa kupatikana na virusi hivyo huku wengine 23 kudaiwa kufariki kutokana na makali ya virusi hivyo kulingana na takwimu za serikali ya Uganda. Wizara ya afya nchini Kenya yaonyesha hofu ya virusi hivyo vya Ebola kukurupuka nchini na kuzitaja kaunti 20 zilizo kwenye hatari zikiwemo :Busia, Machakos, Nakuru, Kiambu, Nairobi, Kajiado, Makueni, Taita Taveta, Mombasa, Kwale, Kericho,Bungoma, Trans Nzoia, West Pokot, Turkana...

FAHAMU MILA YA AJABU NCHINI INDIA YA KURUSHA WATOTO HEWANI.

  Kulingana na wanahistoria wengi , mila ya kutupa mtoto imekuwepo kwa karibu miaka mia saba iliyopita. Zoezi hilo lilianza wakati kiwango cha vifo kati ya Watoto wachanga kilikuwa cha juu sana na hakuna maendeleo ya matibabu yaliyopatikana kuokoa Maisha. Wazazi wa Watoto wachanga wagonjwa au waliokufa walishauriwa na makasisi Fulani kwamba wanapaswa kujenga kaburi na kutupa Watoto wao kutoka urefu wa futi thelathini hadi hamsini. Kulingana na Imani, Mwenyezi angemqwokoa mtotro mchanga.Wazazi wangetupa Watoto wao kutoka juu wakiwa na Imani kubwa kwamba karatasi yenye sura ya machela ingetokea na kunyakua Watoto waowanaoanguka. Japo zoezi hili ni hatari sana hakuna kisa kilichoripotiwa hadi sasa. Ibada hii ilianza kama azimio la ukosefu wa ufahamu wa tiba kwa Watoto wagonjwa na wanaokufa na watu wa mikoa ya Imani na Imani kwa mwenyezi na kuhani. Wazazi wa Watoto waliokuwa wagonjwa na kufa aidha walishauriwa na kasisi kujenga kaburi na kutupa mtoto wao mgonjwa kutoka kwenye paa. Ik...