Kulingana na wanahistoria wengi , mila ya kutupa mtoto imekuwepo kwa karibu miaka mia saba iliyopita. Zoezi hilo lilianza wakati kiwango cha vifo kati ya Watoto wachanga kilikuwa cha juu sana na hakuna maendeleo ya matibabu yaliyopatikana kuokoa Maisha. Wazazi wa Watoto wachanga wagonjwa au waliokufa walishauriwa na makasisi Fulani kwamba wanapaswa kujenga kaburi na kutupa Watoto wao kutoka urefu wa futi thelathini hadi hamsini. Kulingana na Imani, Mwenyezi angemqwokoa mtotro mchanga.Wazazi wangetupa Watoto wao kutoka juu wakiwa na Imani kubwa kwamba karatasi yenye sura ya machela ingetokea na kunyakua Watoto waowanaoanguka. Japo zoezi hili ni hatari sana hakuna kisa kilichoripotiwa hadi sasa.
Ibada hii ilianza kama azimio la ukosefu wa ufahamu wa tiba kwa Watoto wagonjwa na wanaokufa na watu wa mikoa ya Imani na Imani kwa mwenyezi na kuhani. Wazazi wa Watoto waliokuwa wagonjwa na kufa aidha walishauriwa na kasisi kujenga kaburi na kutupa mtoto wao mgonjwa kutoka kwenye paa. Ikiwa kweli wangeamini na kumwamini Mwenyezi, shuka kama chandarua kingetokea angani kwa usalama wao. Mila hii inazua shaka Japo hakuna taarifa za vifo au majeraha ya Watoto kutokana na mila hii.
Ibada inafanywa katika wiki ya kwanza ya Decemba. Zoezi hilo ni la kawaida katika majimbo ya Karnataka na Maharashtra nchini India , haswa katika hekalu la Anathi Digambareshwara na Baba Umer Dargah katika Kijiji cha Nagrala na Sholapur. Zaidi ya familia mia mbili huja kwenye maeneo haya ili Watoto wao wachanga waweze kutupwa kwenye paa.
Ni ibada ya zamani ya kila mwaka iliyofanywa kusini mwa India, iliyokusudiwa kuwaletea Watoto wachanga wanaoshiriki bahati nzuri, afya na ustawi. Picha ambazo ni ngumu kutazama za sherehe hiyo inayofanyika kila mwaka katika jimbo la Karnataka, zimetisha masharika ya kutetea haki za Watoto, na kusema kwamba I ushenzi na hiv
yo basi kutaka mila hii ipigwe marufuku na serikali ya india.
Tamaduni hii inaaminika kuwa na karne za nyuma na inafanyika kote India ikihusisha wahindu na waislamu. Mara baada ya mtoto kuzaliwa, hupelekwa kwenye Darga au hekalu ambako mtoto huwekwa juu ya tone la paa na viungo vyake, akitetemeka na kuhani, na kisha kudondoshwa.
Kundi la watu hungoja chini, wakiwa wameshikilia shuka ili wawavue ndani. Anapokamatwa akiwa salama ndani ya blanketi au shuka, mtoto hupitishwa huku a huko kwa sherehe ya ushindi kabla ya kurudishwa kwa wazazi wake,
Mnamo 2009, majaribio yalifaywa na mamlaka ya wilaya kupiga marufuku tabia hii na bilashaka Ilisimamishwa kwa muda mwaka wa 2011 , lakini mazoezi yalianza tena katika hekalu la Digambareshwara katika Kijiji cha Nagrala mnamo 2012. Ibada ya kurusha mtoto imefanywa kikamilifu hadi maka wa 2016.
Pia kumeibuka picha za matambiko hayo ambapo Watoto hao wanalia, wakionekana kuporomoka kwa futi 30 huku nyuma umati unashangilia, unaonekana kutojali na ukweli kwamba, Watoto hawa wamepitia tukio la kutisha.
Wanakampeni wa ndani walifanikiwa kuharamisha mila hiyo mwaka 2011, lakini ilirejea katika hekalu la Digambeshwara katika Kijiji cha Nagrala kiasi cha kukatishwa tamaa kwa Lov Verma, kutoka tume ya kitaifa ya utetezi wa haki za Watoto.
Bw Verma aliyetoa maneno ya kugadhabishwa na mila hii alisema,” nimeshtuliwa sana na hili.Sio tu kazi ya serikali. Tunahitaji kuwaelimisha wale wote wanaoshiriki hulka hii ya kishenzi.
Nice Article
ReplyDeleteKazi safi💯
ReplyDeleteMila ya kutamausha.
ReplyDeleteKazi nzuri
Interesting
ReplyDeleteKazi safi sana
ReplyDelete