Bilashaka wanasema kila safari huanza na hatua moja na vilevile katika kila hatua hakukosi changamotowe. Chuo kikuu ni mojawapo ya matamanio ya kila mwenye ari ya masomo kufikia ila kupitia vikwazo mbalimbali sio wote hufaulu katika safari hii kwani wengi hulazimika kuachisha safari hii katikati au pia kukosa nafasi kabisa ya kuianza.
Fauka ya hayo, binafsi nimefaulu kuanza masomo kwenye ngazi ya stashahada ya uanahabari katika chuo kikuu cha kiufundi cha Mombasa na kufikia sasa nimekamilisha safari hii kwa asilimia 99. Sio kumaanisha kwamba maisha yamekuwa mtelezo ila changamoto zimekuwepo kiasi cha kukatishwa tamaa na maneno ya wanafunzi wenzangu.
Picha kwa hisani ya Okwonko
Dhana iliyopo kwa wengi walio nje ya masomo ya vyuo vikuu ni kwamba kila mwenye kufika katika chuo kikuu kwa ngazi yoyote, ni mtu mzima na kwa njia moja au nyingine ana uwezo wa kjisimamia kwenye matumizi yake ya kifedha bila ya kumtegemea mtu yeyote wakiwemo wazazi. Ni vigumu kuamini ila katika kujukumika kimasomo ilifikia hatua ya kulazimika kulala bila kutia chochote mdomoni. Ni mtindo ambao haukuwa mpya kwa wanafunzi wengi na hii ni kutokana na kuzorota kwa uchumi hivyo basi kuwatia wategemezi wetu matatani na kupata tabu kuyashugulikia mahitaji yetu kwa ujumla shuleni.
Kupitia kuweko chuoni humu, nimeweza kuimarisha utangamano na uwezo wa kuwa mbunifu haswa kwa hadhira mbalimbali.Ama kweli kwenye taaluma ya uanahabari mtu hupata ujasiri na vilevile uwezo wa kujenga hoja mbele ya watu. Yote haya yamekuwa yenye ufanisi kupitia kuwepo kwa radio ya shule ambayo imekuwa kama njia ya kunolea waandishi wa habari bora wenye natija kwenye jamii kwa ujumla. Binafsi ueledi wangu kwenye kuendesha vipindi hewani umechanguwa sana na kupewa nafasi hewani kwenye radio.
Picha kwa hisani ya Alamin Somo
Vilevile safari nzima haijawa mtelezo tu ila imekuwa na changamoto chungunzima. Suala zima la ukosefu wa usalama limekuwa donda sugu haswa kwa wanafunzi wa chuo kikuu cha kiufundi cha Mombasa. Nikiwa mmoja wa waadhiriwa wa hali kama hii niliyojipata katikati ya wahalifu wenye silaha mbalimbali ikiwemo panga na wengine wao rungu walizokuwa wakininyoshea na kunitishia kuwaachia kifuko nilichokuwa nimebebea kipakatalishi haikuwa rahisi kwangu kuweza kujinasua.
Ni matumaini ya wengi wetu kwamba swala zima la usalama katika kaunti ya Mombasa litatatuliaa japo tuna matumaini sio haba kwamba serikali ya kaunti itaweza kuingililia kati na kuwahakikishia wanafunzi usalama haswa wanapohudhuria vipindi shuleni.
picha kwa hisani ya OkwonkoSasa nina haja ya kujivunia kwani hakuna lililo na mwanzo lisilo na mwisho. Imekuwa ni safari yenye vikwazo vingi na vilevile kujifunza kwingi.Japokuwa sijakata matumaini katika kumalizia safari hii nzima ya uandishi wa habari, kuna haja ya kutia bidii zaidi haswa kwa muda wa takriban mwezi mmoja uliobakia.
Kazi safiiiii
ReplyDeleteGreat
ReplyDeleteKazi safii kijanaa
ReplyDeleteKazi nzuri kabisa,,
ReplyDeleteHongera!!!
Kweli huna budi kufaulu katika maisha👏👏👏
Kazi nzuri
ReplyDelete🔥🔥🔥🔥
ReplyDelete