Skip to main content

PANDASHUKA KATIKA SAFARI YA UANDISHI WA HABARI KATIKA CHUO KIKUU

 Bilashaka wanasema kila safari huanza na hatua moja na vilevile katika kila hatua hakukosi changamotowe. Chuo kikuu ni mojawapo ya matamanio ya kila mwenye ari ya masomo kufikia ila kupitia vikwazo mbalimbali sio wote hufaulu katika safari hii kwani wengi hulazimika kuachisha safari hii katikati au pia kukosa nafasi kabisa ya kuianza.

Fauka ya hayo, binafsi nimefaulu kuanza masomo kwenye ngazi ya stashahada ya uanahabari katika chuo kikuu cha kiufundi cha Mombasa na kufikia sasa nimekamilisha safari hii kwa asilimia 99. Sio kumaanisha kwamba maisha yamekuwa mtelezo ila changamoto zimekuwepo kiasi cha kukatishwa tamaa na maneno ya wanafunzi wenzangu.

Picha kwa hisani ya Okwonko

Dhana iliyopo kwa wengi walio nje ya masomo ya vyuo vikuu ni kwamba kila mwenye kufika katika chuo kikuu kwa ngazi yoyote, ni mtu mzima na kwa njia moja au nyingine ana uwezo wa kjisimamia kwenye matumizi yake ya kifedha bila ya kumtegemea mtu yeyote wakiwemo wazazi. Ni vigumu kuamini ila katika kujukumika kimasomo ilifikia hatua ya kulazimika kulala bila kutia chochote mdomoni. Ni mtindo ambao haukuwa mpya kwa wanafunzi wengi na hii ni kutokana na kuzorota kwa uchumi hivyo basi kuwatia wategemezi wetu matatani na kupata tabu kuyashugulikia mahitaji yetu kwa ujumla shuleni.

Kupitia kuweko chuoni humu, nimeweza kuimarisha utangamano na uwezo wa kuwa mbunifu haswa kwa hadhira mbalimbali.Ama kweli kwenye taaluma ya uanahabari mtu hupata ujasiri na vilevile uwezo wa kujenga hoja mbele ya watu. Yote haya yamekuwa yenye ufanisi kupitia kuwepo kwa radio ya shule ambayo imekuwa kama njia ya kunolea waandishi wa habari bora wenye natija kwenye jamii kwa ujumla. Binafsi ueledi wangu kwenye kuendesha vipindi hewani umechanguwa sana na kupewa nafasi hewani kwenye radio.

Picha kwa hisani ya Alamin Somo


Vilevile safari nzima haijawa mtelezo tu ila imekuwa na changamoto chungunzima. Suala zima la ukosefu wa usalama limekuwa donda sugu haswa kwa wanafunzi wa chuo kikuu cha kiufundi cha Mombasa. Nikiwa mmoja wa waadhiriwa wa hali kama hii niliyojipata katikati ya wahalifu wenye silaha mbalimbali ikiwemo panga na wengine wao rungu walizokuwa wakininyoshea na kunitishia kuwaachia kifuko nilichokuwa nimebebea kipakatalishi haikuwa rahisi kwangu kuweza kujinasua. 

Ni matumaini ya wengi wetu kwamba swala zima la usalama katika kaunti ya Mombasa litatatuliaa japo tuna matumaini sio haba kwamba serikali ya kaunti itaweza kuingililia kati na kuwahakikishia wanafunzi usalama haswa wanapohudhuria vipindi shuleni.

picha kwa hisani ya Okwonko


Sasa nina haja ya kujivunia kwani hakuna lililo na mwanzo lisilo na mwisho. Imekuwa ni safari yenye vikwazo vingi na vilevile kujifunza kwingi.Japokuwa sijakata matumaini katika kumalizia safari hii nzima ya uandishi wa habari, kuna haja ya kutia bidii zaidi haswa kwa muda wa takriban mwezi mmoja uliobakia. 

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

UCHUMI WA WANAMOMBASA BANDARINI

 Halmashauri ya bandari nchini KPA ni moja wapo ya Mashirika ya serikali yanayotoa fursa nyingi za ajira Kwa wafanyikazi wa umma na wa sekta binafsi kushamiri katika taaluma na idara mbalimbali kujipatia riziki. Wanaonufaika pakubwa wakiwa wakaazi wa Kaunti ya Mombasa ambao rasilimali hii iko katika gatuzi Lao.Miongoni mwa biashara zinazodhamiri katika Kaunti ya Mombasa kutokana na uwepo wa banadari ni pamoja na biashara za kupokea mizigo bandarini na kuisafirisha, ile ya magari za kusafirisha mizigo, biashara za hoteli na zingine ndogo ndogo. (Photo courtesy of KPA website) Lakini awali agizo la kuhamishwa Kwa baadhi ya Huduma muhimu za halmashauri hiyo Hadi katika bandari ya nchi Kavu eneo la Naivasha Kaunti ya Nakuru liliwatatiza maelfu ya wafanyikazi kazi wa sekta binafsi hususan madereva wa malori wa kampuni binafsi ambao hutegemea pakubwa kujipatia mapato kupitia kipato kutokana na shughuli ya usafirishaji wa makasha ya mizigo kutoka bandari hiyo Hadi Mataifa mengine...

Mabadiliko ya tabia nchi na athari zake

  Tabia ya nchi ni mwenendo wa hali ya hewa yakiwemo majira, wastani na vizio vya juu na chini kabisa vya joto, utokeaji na mtawanyiko wa mawingu, mvua na theluji, majanga yanayosababishwa na hali ya hewa kama vile upepo mkali na kuanguka kwa theluji, na vimbunga vikali vya nchi kavu na baharini. Tabia ya nchi duniani inabadilika kwa sababu ya kile kinachojulikana kama ‘athari zilizoongezwa nguvu za miali ya jua’. Image Courtesy of google Uhai unawezekana Duniani kwa sababu ya nishati ya jua ambayo hufika katika umbo la mwanga. Dunia huakisi sehemu ya mwanga huu ambao hatimaye hupotelea angani. Hata hivyo, gesi zilizoko kwenye anga hupunguza kasi ya kupotea huku kwa mwanga. Kwa pamoja, gesi hizi hujulikana kama ‘gesi za kuzuia miali ya jua’, kwa Kiingereza, ‘greenhouse gases’, kwani kazi yake ni kuzuia joto lisipotee Duniani. Hii ni kama inavyoonekana katika nyumba maalumu zilizofunikwa kwa nailoni wanazotumia wakulima ili kuotesha mbogamboga. Kiasi fulani cha gesi hizi ni muhimu i...

DHIMA YA VIJANA KATIKA KUIMARISHA UCHUMI WA KENYA

  Hivi karibuni Taifa la Kenya limeingia katika uchumi wa kati ambalo ni jambo muhimu sana katika mtazamo wa kusonga mbele na kuimarisha tena Uchumi wa Taifa hili ambao umelemazwa tangu kuzuka Kwa janga la Covid 19. Photo cortesy of opera Kijana ni mwanajeshi wa mstari wa mbele katika vita ya kiuchumi na hivyo ikiwa kijana hata shiriki katika shughuli za kiuchumi ambazo zina wezesha serikali kuu kukusanya mapato,kijana huyo anakuwa ni mwanajeshi atumikaye kulidondosha Taifa lake kiuchumi hasa ikizingatiwa kuwa anazo nguvu za kutumika katika nafasi ya kulisaidia Taifa lake Kenya kukua kiuchumi ivyo akiwa hatumiki ndani ya Taifa kwa shughuli za kiuchumi atakuwa  analemaza uchumi kwa Taifa. Kijana anapaswa kuzingatia  kuwa kuwa ikiwa kuna kupanda kwa uchumi wa Nchi  pia kuna kushuka kwa uchumi wa Nchi. Hivyo basi tunapokuwa tungali bado vijana na tuna nguvu ni muhimu kujua kuwa uchumi wa Taifa letu lipo mabegani Mwetu . Photo cortesy of nation media Hivyobasi uchumi wa ...