Skip to main content

Mabadiliko ya tabia nchi na athari zake

 

Tabia ya nchi ni mwenendo wa hali ya hewa yakiwemo majira, wastani na vizio vya juu na chini kabisa vya joto, utokeaji na mtawanyiko wa mawingu, mvua na theluji, majanga yanayosababishwa na hali ya hewa kama vile upepo mkali na kuanguka kwa theluji, na vimbunga vikali vya nchi kavu na baharini. Tabia ya nchi duniani inabadilika kwa sababu ya kile kinachojulikana kama ‘athari zilizoongezwa nguvu za miali ya jua’.

Image Courtesy of google

Uhai unawezekana Duniani kwa sababu ya nishati ya jua ambayo hufika katika umbo la mwanga. Dunia huakisi sehemu ya mwanga huu ambao hatimaye hupotelea angani. Hata hivyo, gesi zilizoko kwenye anga hupunguza kasi ya kupotea huku kwa mwanga. Kwa pamoja, gesi hizi hujulikana kama ‘gesi za kuzuia miali ya jua’, kwa Kiingereza, ‘greenhouse gases’, kwani kazi yake ni kuzuia joto lisipotee Duniani. Hii ni kama inavyoonekana katika nyumba maalumu zilizofunikwa kwa nailoni wanazotumia wakulima ili kuotesha mbogamboga.


Kiasi fulani cha gesi hizi ni muhimu ili kutuwezesha kuishi pasipo gesi hizi, wastani wa joto Duniani ungalikuwa nyuzi joto za 19°! Hata hivyo, shughuli za kiuchumi za binadamu (kama vile kilimo, uendeshaji viwanda, na ukataji miti misituni) zinasababisha gesi hizo za kuzuia miali ya jua kuwa nzito zaidi na kwa hiyo kuongeza athari zaidi za miali ya jua Duniani. Ongezeko la joto kwa kawaida hufuatiwa na mabadiliko katika utokeaji wa mawingu, kiasi cha mvua na theluji inayoanguka, mienendo ya pepo na urefu wa majira. Tayari tumeanza kushuhudia baadhi ya mabadiliko haya.

Photo courtesy of google

Kwa sababu mifumo ya hali ya hewa ina miingiliano mingi ya aina yake, mabadiliko ya hali ya hewa yana maana kwamba baadhi ya maeneo duniani hivi sasa yanapata kiwango cha chini cha joto kuliko kawaida, huku maeneo mengine yakipata kiwango cha juu mno na hata mara nyingine kushuhudia hali ya hewa mbaya kupita kiasi, kama vile kupigwa na vimbunga vikali vya nchi kavu na baharini na kughubikwa na dhoruba.


Mwandishi 

Vincent Mutwiri

Comments

  1. Kazi nzuri kabisaa

    ReplyDelete
  2. ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ

    ReplyDelete
  3. Nice work am impressed

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

PANDASHUKA KATIKA SAFARI YA UANDISHI WA HABARI KATIKA CHUO KIKUU

 Bilashaka wanasema kila safari huanza na hatua moja na vilevile katika kila hatua hakukosi changamotowe. Chuo kikuu ni mojawapo ya matamanio ya kila mwenye ari ya masomo kufikia ila kupitia vikwazo mbalimbali sio wote hufaulu katika safari hii kwani wengi hulazimika kuachisha safari hii katikati au pia kukosa nafasi kabisa ya kuianza. Fauka ya hayo, binafsi nimefaulu kuanza masomo kwenye ngazi ya stashahada ya uanahabari katika chuo kikuu cha kiufundi cha Mombasa na kufikia sasa nimekamilisha safari hii kwa asilimia 99. Sio kumaanisha kwamba maisha yamekuwa mtelezo ila changamoto zimekuwepo kiasi cha kukatishwa tamaa na maneno ya wanafunzi wenzangu. Picha kwa hisani ya Okwonko Dhana iliyopo kwa wengi walio nje ya masomo ya vyuo vikuu ni kwamba kila mwenye kufika katika chuo kikuu kwa ngazi yoyote, ni mtu mzima na kwa njia moja au nyingine ana uwezo wa kjisimamia kwenye matumizi yake ya kifedha bila ya kumtegemea mtu yeyote wakiwemo wazazi. Ni vigumu kuamini ila katika ...

UCHUMI WA WANAMOMBASA BANDARINI

 Halmashauri ya bandari nchini KPA ni moja wapo ya Mashirika ya serikali yanayotoa fursa nyingi za ajira Kwa wafanyikazi wa umma na wa sekta binafsi kushamiri katika taaluma na idara mbalimbali kujipatia riziki. Wanaonufaika pakubwa wakiwa wakaazi wa Kaunti ya Mombasa ambao rasilimali hii iko katika gatuzi Lao.Miongoni mwa biashara zinazodhamiri katika Kaunti ya Mombasa kutokana na uwepo wa banadari ni pamoja na biashara za kupokea mizigo bandarini na kuisafirisha, ile ya magari za kusafirisha mizigo, biashara za hoteli na zingine ndogo ndogo. (Photo courtesy of KPA website) Lakini awali agizo la kuhamishwa Kwa baadhi ya Huduma muhimu za halmashauri hiyo Hadi katika bandari ya nchi Kavu eneo la Naivasha Kaunti ya Nakuru liliwatatiza maelfu ya wafanyikazi kazi wa sekta binafsi hususan madereva wa malori wa kampuni binafsi ambao hutegemea pakubwa kujipatia mapato kupitia kipato kutokana na shughuli ya usafirishaji wa makasha ya mizigo kutoka bandari hiyo Hadi Mataifa mengine...