Halmashauri ya bandari nchini KPA ni moja wapo ya Mashirika ya serikali yanayotoa fursa nyingi za ajira Kwa wafanyikazi wa umma na wa sekta binafsi kushamiri katika taaluma na idara mbalimbali kujipatia riziki.
Wanaonufaika pakubwa wakiwa wakaazi wa Kaunti ya Mombasa ambao rasilimali hii iko katika gatuzi Lao.Miongoni mwa biashara zinazodhamiri katika Kaunti ya Mombasa kutokana na uwepo wa banadari ni pamoja na biashara za kupokea mizigo bandarini na kuisafirisha, ile ya magari za kusafirisha mizigo, biashara za hoteli na zingine ndogo ndogo.
(Photo courtesy of KPA website)Lakini awali agizo la kuhamishwa Kwa baadhi ya Huduma muhimu za halmashauri hiyo Hadi katika bandari ya nchi Kavu eneo la Naivasha Kaunti ya Nakuru liliwatatiza maelfu ya wafanyikazi kazi wa sekta binafsi hususan madereva wa malori wa kampuni binafsi ambao hutegemea pakubwa kujipatia mapato kupitia kipato kutokana na shughuli ya usafirishaji wa makasha ya mizigo kutoka bandari hiyo Hadi Mataifa mengine ya Afrika mashariki.
Agizo Hilo jipywa lilipoidhinishwa lilishuritisha makasha hayo yasafirishwe kupitia reli ya kisasa ya SGR. kutokana na agizo hilo
Mara Kwa mara Mashirika ya kutetea Haki za kibinaadamu na wadau wa sekta ya uchukuzi walifanya maandamano wakishinikiza agizo Hilo lilopitishwa na rais mstaafu Uhuru Kenyatta kuondolewa ,wakidai kuwa Hilo liliidhinishwa na maslahi binafsi ya baadhi Mabwenyenye na wala sio Kwa manufaa ya wakenya.
(Photo Cortesy of KPA website)Lakini wakati wa kampeni zake eneo la pwani Aliyekuwa naibu rais kipindi hicho ambaye sasa ni Rais aliyemamlakani William Ruto aliapa kuondoa agizo Hilo siku ya Kwanza mamlakani baada ya kuapishwa rasmi kutekeleza majukumu yake.Ruto alihoji kuwa hatua hiyo ingeimariaha Uchumi wa Kaunti ya Mombasa na pwani nzima Kwa ujumla ambao ulionekana kudorora Kufuatia agizo lilolwekwa na mtangulizi wake Uhuru Kenyatta.
Siku ya Kwanza ya kuapishwa kwake rais William Ruto alitia sahihi ya kiuentendaji amri ya kuregeshwa Kwa oparesheni zote kutoka Eneo la Naivasha Hadi Kaunti ya Mombasa. Hatua hii ilipokelewa vyema na madereva wa masafa marefu, wauzaji wa vipuri vya magari pamoja na wafanyibiashara wengi wanaofaidika kutokana na shughuli za bandari.
Licha ya kuwa agizo limeanza kutekeleza minong'ono imeibuka kuwa baadhi ya wakurugenzi katika halmashauri hiyo KPA wanashuritisha mizigo ya inayosafirishwa Taifa la Sudan Kusini kuidhinishwa katika mabohari binafsi Jambo ambalo limekewa vikali na wadau wa sekta ya uchukuzi kutoka Mataifa la Sudan Kusini na Kenya.
MWANDISHI
VINCENT MUTWIRI
Kazi safiiiii mkuu
ReplyDeleteKazi msury mkuuu 🔥🔥🔥
ReplyDeleteKazi safi kaka
ReplyDeleteKazi safi
ReplyDeleteKazi safi kiswahili chenyewe daah
ReplyDeleteKiswahili kimekubali aisee
ReplyDeleteThank you
Deletenakala safi
ReplyDeleteNice one
ReplyDeleteKazi murwa mkurugenzi👍🙏
ReplyDeleteThank you
DeleteKazi murwa mkurugenzi👍🙏
ReplyDeleteNakala nzuri
ReplyDeleteThank you
Delete🔥🔥🔥🔥🔥
ReplyDeleteThank you
DeleteKazi safi
ReplyDeleteThank you
DeleteKazi safi kabisa
ReplyDeleteKazi nzuri
ReplyDeleteThank you
DeleteKazi safi
ReplyDeleteGood job
ReplyDeleteThank you
DeleteKazi safi...hongera mkuu
ReplyDelete