Skip to main content

UCHUMI WA WANAMOMBASA BANDARINI

 Halmashauri ya bandari nchini KPA ni moja wapo ya Mashirika ya serikali yanayotoa fursa nyingi za ajira Kwa wafanyikazi wa umma na wa sekta binafsi kushamiri katika taaluma na idara mbalimbali kujipatia riziki.

Wanaonufaika pakubwa wakiwa wakaazi wa Kaunti ya Mombasa ambao rasilimali hii iko katika gatuzi Lao.Miongoni mwa biashara zinazodhamiri katika Kaunti ya Mombasa kutokana na uwepo wa banadari ni pamoja na biashara za kupokea mizigo bandarini na kuisafirisha, ile ya magari za kusafirisha mizigo, biashara za hoteli na zingine ndogo ndogo.

(Photo courtesy of KPA website)

Lakini awali agizo la kuhamishwa Kwa baadhi ya Huduma muhimu za halmashauri hiyo Hadi katika bandari ya nchi Kavu eneo la Naivasha Kaunti ya Nakuru liliwatatiza maelfu ya wafanyikazi kazi wa sekta binafsi hususan madereva wa malori wa kampuni binafsi ambao hutegemea pakubwa kujipatia mapato kupitia kipato kutokana na shughuli ya usafirishaji wa makasha ya mizigo kutoka bandari hiyo Hadi Mataifa mengine ya Afrika mashariki.


Agizo Hilo jipywa lilipoidhinishwa lilishuritisha makasha hayo yasafirishwe kupitia reli ya kisasa ya SGR. kutokana na agizo hilo

Mara Kwa mara Mashirika ya kutetea Haki za kibinaadamu na wadau wa sekta ya uchukuzi walifanya maandamano wakishinikiza agizo Hilo lilopitishwa na rais mstaafu Uhuru Kenyatta kuondolewa ,wakidai kuwa Hilo liliidhinishwa na maslahi binafsi ya baadhi Mabwenyenye na wala sio Kwa manufaa ya wakenya.

(Photo Cortesy of KPA website)

Lakini wakati wa kampeni zake eneo la pwani Aliyekuwa naibu rais kipindi hicho ambaye sasa ni Rais aliyemamlakani William Ruto aliapa kuondoa agizo Hilo siku ya Kwanza mamlakani baada ya kuapishwa rasmi kutekeleza majukumu yake.Ruto alihoji kuwa hatua hiyo ingeimariaha Uchumi wa Kaunti ya Mombasa na pwani nzima Kwa ujumla ambao ulionekana kudorora Kufuatia agizo lilolwekwa na mtangulizi wake Uhuru Kenyatta.


Siku ya Kwanza ya kuapishwa kwake rais William Ruto alitia sahihi ya kiuentendaji amri ya kuregeshwa Kwa oparesheni zote kutoka Eneo la Naivasha Hadi Kaunti ya Mombasa. Hatua hii ilipokelewa vyema na madereva wa masafa marefu, wauzaji wa vipuri vya magari pamoja na wafanyibiashara wengi wanaofaidika kutokana na shughuli za bandari.


Licha ya kuwa agizo limeanza kutekeleza minong'ono imeibuka kuwa baadhi ya wakurugenzi katika halmashauri hiyo KPA wanashuritisha mizigo ya inayosafirishwa Taifa la Sudan Kusini kuidhinishwa katika mabohari binafsi Jambo ambalo limekewa vikali na wadau wa sekta ya uchukuzi kutoka Mataifa la Sudan Kusini na Kenya.


MWANDISHI

VINCENT MUTWIRI

Comments

  1. Kazi msury mkuuu 🔥🔥🔥

    ReplyDelete
  2. Kazi safi kiswahili chenyewe daah

    ReplyDelete
  3. Kazi murwa mkurugenzi👍🙏

    ReplyDelete
  4. Kazi murwa mkurugenzi👍🙏

    ReplyDelete
  5. Kazi safi...hongera mkuu

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

Mabadiliko ya tabia nchi na athari zake

  Tabia ya nchi ni mwenendo wa hali ya hewa yakiwemo majira, wastani na vizio vya juu na chini kabisa vya joto, utokeaji na mtawanyiko wa mawingu, mvua na theluji, majanga yanayosababishwa na hali ya hewa kama vile upepo mkali na kuanguka kwa theluji, na vimbunga vikali vya nchi kavu na baharini. Tabia ya nchi duniani inabadilika kwa sababu ya kile kinachojulikana kama ‘athari zilizoongezwa nguvu za miali ya jua’. Image Courtesy of google Uhai unawezekana Duniani kwa sababu ya nishati ya jua ambayo hufika katika umbo la mwanga. Dunia huakisi sehemu ya mwanga huu ambao hatimaye hupotelea angani. Hata hivyo, gesi zilizoko kwenye anga hupunguza kasi ya kupotea huku kwa mwanga. Kwa pamoja, gesi hizi hujulikana kama ‘gesi za kuzuia miali ya jua’, kwa Kiingereza, ‘greenhouse gases’, kwani kazi yake ni kuzuia joto lisipotee Duniani. Hii ni kama inavyoonekana katika nyumba maalumu zilizofunikwa kwa nailoni wanazotumia wakulima ili kuotesha mbogamboga. Kiasi fulani cha gesi hizi ni muhimu i...

DHIMA YA VIJANA KATIKA KUIMARISHA UCHUMI WA KENYA

  Hivi karibuni Taifa la Kenya limeingia katika uchumi wa kati ambalo ni jambo muhimu sana katika mtazamo wa kusonga mbele na kuimarisha tena Uchumi wa Taifa hili ambao umelemazwa tangu kuzuka Kwa janga la Covid 19. Photo cortesy of opera Kijana ni mwanajeshi wa mstari wa mbele katika vita ya kiuchumi na hivyo ikiwa kijana hata shiriki katika shughuli za kiuchumi ambazo zina wezesha serikali kuu kukusanya mapato,kijana huyo anakuwa ni mwanajeshi atumikaye kulidondosha Taifa lake kiuchumi hasa ikizingatiwa kuwa anazo nguvu za kutumika katika nafasi ya kulisaidia Taifa lake Kenya kukua kiuchumi ivyo akiwa hatumiki ndani ya Taifa kwa shughuli za kiuchumi atakuwa  analemaza uchumi kwa Taifa. Kijana anapaswa kuzingatia  kuwa kuwa ikiwa kuna kupanda kwa uchumi wa Nchi  pia kuna kushuka kwa uchumi wa Nchi. Hivyo basi tunapokuwa tungali bado vijana na tuna nguvu ni muhimu kujua kuwa uchumi wa Taifa letu lipo mabegani Mwetu . Photo cortesy of nation media Hivyobasi uchumi wa ...