Tabia ya nchi ni mwenendo wa hali ya hewa yakiwemo majira, wastani na vizio vya juu na chini kabisa vya joto, utokeaji na mtawanyiko wa mawingu, mvua na theluji, majanga yanayosababishwa na hali ya hewa kama vile upepo mkali na kuanguka kwa theluji, na vimbunga vikali vya nchi kavu na baharini. Tabia ya nchi duniani inabadilika kwa sababu ya kile kinachojulikana kama ‘athari zilizoongezwa nguvu za miali ya jua’. Image Courtesy of google Uhai unawezekana Duniani kwa sababu ya nishati ya jua ambayo hufika katika umbo la mwanga. Dunia huakisi sehemu ya mwanga huu ambao hatimaye hupotelea angani. Hata hivyo, gesi zilizoko kwenye anga hupunguza kasi ya kupotea huku kwa mwanga. Kwa pamoja, gesi hizi hujulikana kama ‘gesi za kuzuia miali ya jua’, kwa Kiingereza, ‘greenhouse gases’, kwani kazi yake ni kuzuia joto lisipotee Duniani. Hii ni kama inavyoonekana katika nyumba maalumu zilizofunikwa kwa nailoni wanazotumia wakulima ili kuotesha mbogamboga. Kiasi fulani cha gesi hizi ni muhimu i...