Bilashaka wanasema kila safari huanza na hatua moja na vilevile katika kila hatua hakukosi changamotowe. Chuo kikuu ni mojawapo ya matamanio ya kila mwenye ari ya masomo kufikia ila kupitia vikwazo mbalimbali sio wote hufaulu katika safari hii kwani wengi hulazimika kuachisha safari hii katikati au pia kukosa nafasi kabisa ya kuianza. Fauka ya hayo, binafsi nimefaulu kuanza masomo kwenye ngazi ya stashahada ya uanahabari katika chuo kikuu cha kiufundi cha Mombasa na kufikia sasa nimekamilisha safari hii kwa asilimia 99. Sio kumaanisha kwamba maisha yamekuwa mtelezo ila changamoto zimekuwepo kiasi cha kukatishwa tamaa na maneno ya wanafunzi wenzangu. Picha kwa hisani ya Okwonko Dhana iliyopo kwa wengi walio nje ya masomo ya vyuo vikuu ni kwamba kila mwenye kufika katika chuo kikuu kwa ngazi yoyote, ni mtu mzima na kwa njia moja au nyingine ana uwezo wa kjisimamia kwenye matumizi yake ya kifedha bila ya kumtegemea mtu yeyote wakiwemo wazazi. Ni vigumu kuamini ila katika kuju