Skip to main content

Posts

Showing posts from September, 2022

HOFU YA EBOLA NCHINI KENYA

 Kufuatia kudhibitishwa kuwepo kwa virusi vya Ebola nchini Uganda mnamo tarehe 19 mwezi wa tisa 2022 , wizara ya afya nchini humo sasa yawataka waadhiriwa licha ya kupokea matibabu, kuepuka tendo la ndoa angalau kwa siku tisini. Haya yanajiri baada ya kubainika kwamba virusi hivi bado vinaenea hata baada ya muadhiriwa kupokea matibabu hivyo basi kusambazwa sio kwa njia ya mate na damu pekee ila wanasayansi sasa wanabaini kuna uwezekano wa virusi hivyo kupatikana kwenye manii (semen) ya mwanaume hata baada ya kupata matibabu dhabiti. Haya yaanjiri baada ya watu 36 kudaiwa kupatikana na virusi hivyo huku wengine 23 kudaiwa kufariki kutokana na makali ya virusi hivyo kulingana na takwimu za serikali ya Uganda. Wizara ya afya nchini Kenya yaonyesha hofu ya virusi hivyo vya Ebola kukurupuka nchini na kuzitaja kaunti 20 zilizo kwenye hatari zikiwemo :Busia, Machakos, Nakuru, Kiambu, Nairobi, Kajiado, Makueni, Taita Taveta, Mombasa, Kwale, Kericho,Bungoma, Trans Nzoia, West Pokot, Turkana na